Aliyekuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
SPIKA wa bunge la Zimbabwe, Jacob Mudenda jioni ya leo ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu.
Spika huyo amesema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo
ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko mazuri ya mamlaka kulingana na chombo
cha habri cha reuters.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng’oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.
Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.
Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua
mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka
kiongozi huyo kung’atuka mamlakani wiki hii.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment