Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa
hajawahi kupata barua yoyote kutoka CCM inayomfukuza unanacha kama
inavyodaiwa.
Mh. Nyalandu ameiambia Bongo5 leo, kuwa ndani ya
chama hicho huwa kuna utaratibu na hawamfukuzi mtu kwa barua bali kuna
kuwa na vikao vinavyohusiana na maadili hivyo basi amesema tangu awe
ndani ya chama hicho hakuna kikao kilichowahi muita kuhusiana na masuala
ya maadili.
“Wakati najiuzulu tarehe 30 mwezi Oktoba, nilifanya hivyo kwa nia yangu mwenyewe na kwa uamuzi wangu mwenyewe, sikuwa nimepata barua yoyote kutoka CCM inayonifukuza, kwahiyo dhana ya kwamba kulikuwa na barua yakunifukuza uanachama sio kweli lakini vilevile ikumbukwe kwamba mimi sikuwa mwananchama wa kawaida mimi nilikuwa ni mbunge ana jimbo pili nilikuwa ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na utaratibu wa chama chetu haufukuzwi tu kwa barua huwa kuna vikao vinavyohusiana na maadili huwa vinakaa,” amesema Nyalandu.
“Hakuna kikao chochote tangu niwe mwananchama ambacho kiliwashawahi kuniita kuhusiana na masuala yanayohusiana na maadili, kwahiyo mimi naona tungejikita tu kufanya muktabari wa nchi yetu tufanye siasa za ushindani na turuhusu watu wawe huru na tusisababishe malumbano ambayo hayana sababu yoyote,”ameongeza.
Nyalandu Jumatatu hii ya tarehe 30 Oktoba mwaka huu aliamua kukihama chama cha Mapinduzi (CCM) na kujivua ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment