Msanii wa muziki Bongo, M2 The P amewatolewa uvivu wasanii wanaondekeza kiki hadi kusahau kufanya muziki wao.M2 The P ameseme iwapo msanii anafanya hivyo awe na kazi nzuri zinazoeleweka na siyo kiki tu wakati hata kazi zake hazionekani.
“Kwangu kiki hazina umuhimu sana cha muhimu ni kufanya kitu kizuri,
kiki zinakuja tu baadae, siwezi nikafanya kiki mwishoe ikaja kuniletea
matatizo lakini ukifanya kitu kizuri kwenye muziki mzuri watu wataupokea
tu,” M2 The ameiambia Bongo5.
“Kuna wasanii wameshakuwa katika mfumo ambao hawezi kutoa wimbo bila
kiki, kiki nyingi halafu halfu mimi huwa sizifuatilii ni maneno tu
ambayo huwa yanaongelewa mtaani na kupita” ameongeza.
Katika hatua nyingine M2 The P amesema yupo mbioni kutoa ngoma mpya
baada ya ile ‘Nakuhonga’ ambayo alimshirikisha Mr. Blue iliyotoka miezi
saba iliyopita.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment