
Mkurugenzi wa kundi la Unit Family Deoglasi Rusinde akizungumza kwenye ukumbi wa kituo cha Amani kilichopo Chamwino Morogoro

Mkurugenzi wa kundi la Unit Family
Deoglasi Rusinde akimkabidhi zawadi mbali mbali Afisa Ustawi wa Jamii
Kituo cha Amani Bw SalvatoryAugustino[kulia]

Baada ya kutoka Kituo ya Mehayo
Mazimbu na baadae kituo cha Aman Chamwino kundi la Unit Family lilitia
timu kituo cha Erick kilichopo Kiwanja cha Ndege eneo la Nanasi


Ukibahatika kuingia mbinguni na
usipomuona pepeponi Mama Josephini Bakhita unaweza kumhoji Mungu kwamba
kwa nini Mama huyo hayupo Peponi kwa matendo mazuri aliyoyafanya
duniani? Mama Makhita ambaye katika maisha yake alibahatika kupta mtoto
tu Erick Samanka mwenye ulemavu wa Viungo na akili.
Akizungumza na Mtandao huu Mama
Makhita alisema baada ya kumzaa mwanae akiwa na hali hiyo mwaka 1992
aliamua kuanzisha kituo cha Amani na kuwalea watoto wengine wenye
matatizo kama ya Mwanae.
" baada ya kuanzishi kituo hicho mwaka
huu 92 nilipokea watoto wengi na kujikuta nikielemewa na majukumu ya
kuwalisha na kuwatibu hivyo niliamua kukigawa kituo hicho kwa kanisa
Katoliki Jimbo la Morogoro
" Mwaka 2003 Mwanangu Erick aliaga
dunia na mwaka 2009 nikiwa mtumishi wa serikali nilistaafu kazi na
kujaliwa kujenga hii nyumba nikawiwa nikaamua kuanzishi kituo kingine
hapa hapa nyumbani nilichokipa jina la Marehemu Mwangu Erick kwa sasa
naishi na watoto 16 wenye matatizo mbali mbali''alisema mama huyo

Mama alisema miongoni mwa watoto hao
16 yuko mtoto wa kimasai Joel Yona[10] " Huyu mtoto alizaliwa akiwa na
ulemavu wa akili na Viungo haqwezi kukaa wala kusimama mwingi analia
maumivu. " Huyu baada ya kuzaliwa na hali hii wazazi wake walimtelekeza
Mstuni kule Mvomero nikapata taarifa akapanda gari na kwenda kumchukua
na kuishi naye hapa"alisema Mama huyo na kuongeza.
" Kati ya walemavu duniani kote
walemavu hawa wenye ulemavu wa viungo na akili wanahitaji upendo na
uangalizi wa karibu sana kwani ni tofauti na walemavu wengine ambao
wanaweza kupambana na hali zao na kwenda nyumba za lbada au kwenye
maduka mijini kuomba msaada tofauti na hawa ambao akili ya kutambua hilo
hawana vile vile uwezo wa kutembea hawana"alisema mama huyo jambo
lililoamsha vilio kutoka kwa watu waliokuwepo kanisani hapo pamoja na
Askofu na mkewe


Mama Makhita akitoka histori ya Mtoto
huyo huku mtoto huyo akiangua kilia akilalamika maumivu, kitendo
kilichowaliza wanafamilia wa kundi la Unit

Wanachama wa Uniti wakiangua vilio

Hebu cheki video ya tukio hilo

Mtoto Joel akishushwa kwenye kifaa chake cha kisimamia

Watoto Joel[10] Kulia na Grece
Emmanuel[17] wakiwa na walezi wao. licha ya umri mkubwa Grece anaonekana
kuwa an sawa na Joel kufuatia kusumbuliwa na maradhi.

Mkurugenzi wa Uniti family Deoglas
Rusinde[kulia kwa kushirikiana na Katibu wa kanisa la EAGT Sayuni Temple
Bw Whery Lyimo Wakimkabidhi zawadi Mama Makhita

Kundi la Uniti Falmily wakipiga Picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Erick

.... Baada ya kukabidhi zawadi hilo wana Unit Family waliangusha maombi kwa watoto hao

.....Mwandishi wa Mtandao huu mwenye flana ya mistari akishiriki kuangusha maombi kwa watoto hao

Baada ya maombi kukalea Mtoto huyu alipandwa na mapepo



Baada ya kutoka Kituo cha Erick
Mwandishi wa Mtandao huu alitinga ofisni kwa Askofu wa Kanisa la EAGT
Satubi Tenple Askofu Peter Denis na kufanya naye mahojiano ofisini
kwake

Kanisa la EAGT Sayi=uni Temple lililopo Pande za Chwamino Morogoro



Mkurugenzi wa Unit Family ]kati]
akizungumza ofisni kwa Askofu Densi kabla ya Tamasha hilo kuanza[
kushoto na Mgeni rasm Bw Fiume na kulia ni Askofu Denis



Mama Makhita akifika kanisani hapo na mwane Joel
Waasisi wa Vituo vya kulelea watoto
wenye matatizo mbali mbali Josephini Bakhita[kushoto] kituo cha Aman na
Rinda Ng'ido wa kituo cha Mehayo Mazimbu
Mama Rinda akizungumza
Mama Bakhita akizungumza kanisani hapo
Askofu Denisi aliamulu kanisa lote kiweka mikoto juu ya watoto hao wakati akiwafanya maombi
Watoto Joel kushoto na Grece kulia wakipokea maombi kutoka kwa Askofu
Maneno yaliyokuwa yakitamkwa kwenye
maombi hayo yaliwaliza wengi kanisani hapo ambapo Mwandishi wa Mtandao
huu pia alishindwa kuzuia chozi lake na kumwagika
Mke wa Askofu Denis Bi, Mwamini Denisi naye akimwaga chozi wakati mumewe akiwaombe watoto hao
...Baada ya Maombi na kushuhudia sehemu kubwa ya kanisa wakiangua vilio Askofu Denis alijikuta naye akitokwa na chozi
MUNGU ni mwema baada ya maombi hayo
mazito maumivu ya Mtoto Joel yalipungua kama alivyonasw ana kamera ya
mtandao huu kanisani hapo
Baada ya maombi viongozi hao walikata keki na kula na watoto hao
......Wakiikata keki
....Mgeni rasm akimrisha mmoja wawato hao
...Askofu akimrisha keki mgeni rasm
Mama Askofu akimrisha keki mumewe
Bingwa wa salam redio Tanzania Matata
Ndizi ambaye ni mwanachama Pekee wa kundi la Unit Family kutoka nje ya
Dar akihojiwa na Mtandao huu. lfahamike Matata Ndizi ni mfanyabiashara
wa Soko Mkuu Morogoro
Kiongozi wa kundi la Unit Family
akimkabidhi baiskel 2 mgeni rasm ambaue naye alikabidhi zawadi hizi kwa
mmiliki wa kituo cha Mehayo Mama Rinda
Stori: Dunstan Shekidele,Morogoro
Mtoto
wa kimasai aliyetupwa na wazazi wake baada ya kuzaliwa akiwa na
ulemavu wa viungo na akili , Joel Yona (10) ambaye hawezi kukaa wala
kusimama, amewaliza wengi akiwemo Askofu Peter Denis wa Kanisa la EAGT
Sayuni Temple lililipo Chamwino mjini hapa.
Wiki
iliyopita, katika kuadhimisha miaka 7 tangu kuanzishwa kwa kikundi cha
Unit Family kutoka jijini Dar, kinachojihusisha na utoaji misaada kwa
watu wenye mahitaji maalum, kiliamua kufika Mkoani hapa kutembelea vituo
vya watoto mbalimbali.
Miongoni
mwa vituo walivyotembelea ni kituo cha Mehayo kilichopo Mazimbu, Aman
kilichopo Chamwino na Erick kilichopo kiwanja cha Ndege ambapo Unit
Familly waliwaalika watoto wote wa Vituo hivyo kwenye tamasha
lilifanyika kanisani hapo.
Katika
Tamasha hili ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dr.
Kebwe Stephen Kebwe aliyewakilishwa na Afisa Biashara wa Manispaa ya
Morogoro, Mfaume Fiume, wanachama zaidi ya 20 wa Unit Familly walikula
na kunywa na watoto hao na baadae kukabidhi zawadi kwa watoto zikiwemo
baiskeli mbili za matairi.
Awali,
Unit Familly waliguswa zaidi na kujikuta wakiangua vilio baada ya
kutembelea kituo hicho cha Erick na kuguswa na ugonjwa na historia ya
mtoto Joel,.
Aidha,
mbali na maradhi na historia ya Joel pia waliguswa na mwezake Grace
Emmanuel (17) ambaye naye historia ya maisha yake illitolewa kanisani
hapo na mlezi wao Josephine Bakhita.
Akizungumza
kwenye tamasha hilo, Askofu Denis alisema: "Naamini Mungu anaweza
kuwaponya watoto hawa hata sasa hivi, lakini ana kusudi maalum la
kuwaacha kuwa walivyo".
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Fiume alisema: "Serikali ya Mkoa wa
Morogoro inatambua uwepo wa vituo hivyo vitatu na kupitia tamasha hili
tutaongeza juhudi za kuvihudumia vituo hivyo"
Kwa upande wake mkurugenzi wa Unit Family Deoglas Rusinde ambaye pia
ni Produse wa kipindi cha Njia Pande Radio Clouds alisema.
”
Kundi letu la Unit Family linalojihusisha na utaoaji misaada kwa watu
wenye uhitaji maalumu kwa wanakikundi kujichangisha limetimiza miaka 7
toka kuanzishwa hivyo tumeona Mwaka huu tuje morogoro kujumuika na watu
wenye matatizo mbali mbali”alisema Mkurugenzi huyo
Katika
Tamasha hilo waimbaji Maarufu wa ijiniri kutoka Dar na Moro walipafomu
akiwemo dereva Maarufu wa SUA Mzee Tegemea Leonald.
Picha za waimbaji hao zitawajia hivi punde endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment