Akizungumza na wana habari mtu wa karibu na askari hao amesema kuwa chanzo cha ugomvi wa askari hao ni wivu wa mapenzi ambapo marehemu pamoja na mtuhumiwa ambaye ametambulika kwa jina la Faustine Masanja wameona nyumba moja.
Amedai marehemu alipofika asubuhi kazini ndipo mtuhumiwa Masanja alimpiga mwenzake risasi ya kichwa na alipokimbizwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru alifariki dunia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha hilo na kusema tukio hilo limetokea asubuhi wakati askari hao wakiwa kazini na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mkoa Mount Meru.
Aidha Kamanda Mkumbo amedai kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment