December 14, 2017

Image result for godbless lema leo
Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema amefunguka na kusema ahadi ambazo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakipewa jambo linalopelekea kujiuzulu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Lema amesema hayo leo Disemba 14, 2017 mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baadhi ya vyama vya upinzani nchini vimekuwa vikikumbana na changamoto ya baadhi ya viongozi wao au wananchama kujivua uanachama na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile wanachodai wanaunga mkono juhudi na utendaji kazi wa Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli.

 Image may contain: 1 person, text

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE