December 13, 2017


 
 Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amefunguka na kusema kuwa anakwenda mjini Dodoma kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa ngazi za juu wa chama.
Ridhiwani Kikwete amedai kuwa kura yake kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa itakwenda kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli 
"Ninakwenda Dodoma Kwenye Mkutano Mkuu kuchagua Viongozi wa Juu wa Chama Changu. Kura yangu ya Mwenyekiti nitamchagua Dr.John Magufuli.. Nakuomba nawe kura kwake" alindika Ridhiwani Kikwete 

Mkutano Mkuu wa Taifa wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) unatarajiwa kuanza Disemba 15, 2017 ambapo pamoja na mambo mengine watafanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa ngazi ya juu ya chama hicho.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE