Idara ya Uhamiaji nchini imesema sakata la kumuhoji uraia wake Askofu wa
Jimbo la Ngara , Severine Niwemugizi, wataweka wazi pindi uchunguzi
utakapokamilika.
Hayo amesema jana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Makakala.
''Hizo ni taarifa za
kiuchunguzi ambazo bado tunaendelea nazo, huwezi kuweka wazi kila kitu
wakati bado tupo katika uchunguzi, tunapokuwa na shaka na mtu yoyote
kuhusu uraia wake tunaruhusiwa kumuhoji,'' amesema Dr. Makakala.
Madai ya Askofu huyo kuhusu
kuhoji upatikanaji wa katiba mpya ndio sababu ya kuhojiwa na idara
hiyo, Dr. Anna amekanusha na kusema wawaache kwanza hadi uchunguzi
utakapokamilika.
''Hayo ya kwake, naomba tusubiri uchunguzi hadi utakapo kamilika,'' ameongeza
0 MAONI YAKO:
Post a Comment