Amesema kilichopo kati ya Alikiba na Diamond ni ushindani wa kimuziki kitu ambacho ni kizuri katika ukuaji wa muziki wa Bongo Flava.
“Siwezi kusema wana beef labda wana ushindani wa muziki, kila mtu anajali kufanya kazi vizuri, Mungu awalijie waendelee kufanya vizuri, sitaki beef waendelee tu muziki wetu ufike mbali” M 2 The P ameiambia Bongo5.
M 2 The P amemtolea mfano Diamond kwa kusema ameweza kufanya kolabo na wasanii wengi wa kimataifa kitu ambacho kimeitangaza Afrika Mashariki kimuziki na ndivyo inavyotakiwa na siyo beef.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment