Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA,amabye pi ni mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya cha hicho John Mnyika amejitoa kizalendo kwa kuwaombea askari
14 wa JWTZ ambao wamefariki dunia nchini Congo wakati wakilinda amani
huku askari wengine 44 wakiwa wamejeruhiwa.
Mbunge wa Kibamba ameitumia Jumapili ya leo Disemba 10,2017 kuwaombea mashujaa hao na kuwapa pole wanafamilia wote ambao ndugu zao wamepoteza maisha katika tukio hilo.
Mbunge wa Kibamba ameitumia Jumapili ya leo Disemba 10,2017 kuwaombea mashujaa hao na kuwapa pole wanafamilia wote ambao ndugu zao wamepoteza maisha katika tukio hilo.
"Kwa kipekee naitoa ibada ya leo kuwaombea Mashujaa
wetu,askari 14 wa JWTZ waliojitoa mhanga na maisha yao kuitetea amani
Congo, 44 ambao wamejeruhiwa na wale wawili (2) ambao hawajulikani
walipo. Mungu awajalie pumziko jema kwa wale waliopoteza uhai kupigania
amani"
Mnyika aliendelea kusema kuwa
"Awape uponyaji majeruhi na kusaidia kupatikana kwa
Askari wawili. Aijalie faraja na ustawi familia za wahanga na wote ambao
wameguswa kwa moja kwa moja au namna ingine yeyote na tukio baya hilo" aliandika John Mnyika
0 MAONI YAKO:
Post a Comment