December 16, 2017

Image result for Zitto Kabwe
Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo na mbunge wa kigoma, Zuberi kabwe Zitto amesema kuwa chama chake kitaendelea kuikosoa serikali pale ambapo mambo hayaendi na kuipongeza pale yanapoenda sawa maana kufanya hivyo n jambo la muhinu na la kizalendo.
Akizungumza na waandishi leo katika makao makuu ya chama hicho kijitonyama, amesema kuwa kusiogopwe kuikosoa serikali kwa hoja maana n uzalendo.
Katika kikao hicho cha kamati kuu wameongelea mambo makuu mawili, Hali ya siasa ndani na nje ya chama mfumo wa kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na hali ya uchimi wa nchi.
Amewashukuru wajumbe wa kamati kuu kwa utulivu na ukomavu wanaouonyesha licha ya mawimbi wanayopitia kwa baadhi yao kuhamia vyama vingne na kuendelea kuwamshambulia kwa namna tofauti ila wao wanaendelea kuwa watulivu na kusonga mbele.
Amesema kwa sababu ya wao kuhamia chama tawala kutoka vyama vya upinzan kuwa wanaunga juhudi za Rais hiyo sababu haitoshi kuelezea maamuzi yao.
Chama cha ACT wazalendo n lazima kiendelee kuunga mkono juhudi za Rais na zozote za kuondoa ufisadi nchin mwetu, na mm kama kiongoz wao na mara nyingi huwa nasifia pale napoona panafaa na kukosoa pale pasipofaa,
“Wenzetu wana sababu zaidi ya kumuunga mkono Rais” amesema Zitto.
Aidha katika hali ya uchumi wa nchi amesema repot ya shirika la fedha la kimataifa (IMF) limeitaka serikali kutazama upya vyanzo vyake vya takwimu za uchumi iki kupata picha ya hali ya uchumi wa Taifa.
“Jambo muhimu ambalo watu wa IMF wameiambia serikali n suala la kuheshimu bajet” Zitto.
Pia ameishauri kamati kuu kutoa azimio kuwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikal kufanya ukaguzi maalum na kutoa taarifa ili Bunge kuwachukulia hatua maafisa wote wa serikal wanaokiuka sheria za matumiz ya fedha bila kujali vyeo vyao.
Ameipongeza serikal kwa kuchukua wazo lao la kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ili kubakia mitatu, miwil ya pensheni na mmoja mfuko taifa wa bima ya afya.
Lakin amesema muswaada unaopendekezwa Bungen una matatizo yanayoweza kusababisha wazee na wastaafu zaidi ya 120,000 kukosa kabisa pensheni zao mara tu baada ya muswaada huo kupitishwa na kuwa sheria.
Ameiomba pia kamati kuu kuazimia chama kuanza kazi ya kuhamasisha makundi ya vyama vya wafanyakazi nchini kuungana na kusimamia pamoja kupinga mswaada huo ili kuboresha na kulinda maslahi ya wazee wetu wastaafu.
“Mswaada huo utaharibu maisha ya watanzania wenzetu 120,000 pamoja na wategemezi wao” amesema Zitto.
Aidha amegusia pia mswaada wa sheria mpya ya vyama vya siasa nchini kuwa ukiachwa na kuwa sheria utafuta siasa za vyama vingi nchini.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE