STAA
wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kipekee, Elias Barnaba amesema kuwa
kitendo cha kuwatungia mastaa ngoma zao hasa wa kike kimemfanya
kutengeneza mkwanja mrefu.
Akichonga na Risasi Vibes, Barnaba ambaye kwa sasa
amejitoa THT na kuanzisha lebo yake ya Hightable Sound alisema, hawezi
kutaja mpaka sasa amepata kiasi gani lakini wasanii wa kike wengi
aliowatungia ngoma wamekuwa wakimlipa vizuri.
“Ukiachilia mbali mkwanja ninaoupata kupitia studio na lebo yangu ya
Hightable, kazi zangu za muziki, kingine kikubwa ni hawa wasanii
ninaowatungia nyimbo, wamekuwa wakinipa mkwanja mrefu,” alisema Barnaba
ambaye amewahi kuwatungia nyimbo mastaa kibao wa kike akiwemo Linah,
Shilole, Lulu Diva, Recho na wengineo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment