
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Februari 21, 2018 itatoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya
inayomkabili Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa
na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya upande wa mashtaka
ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kuwaita mashahidi
watatu kutoa ushahidi dhidi ya Masogange na kuufunga na mshtakiwa mwenyewe
kujitetea
Akiongozwa na Mawakili Nehemiah
Nkoko na Ruben Simwanza kutoa utetezi wake leo Masogange ameiomba Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote
Masogange anakabiliwa na
kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, katika utetezi
wake amedai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja
Akijitetea Masogange alidai kuwa
mbali ya ‘Uvideo Queen’ pia alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo.</p></div><div><p>Alidai
kuwa Februari 14,2017 polisi walienda nyumbani kwake, yeye hakuwepo, alikuwepo
dada yake, yeye alikuwa amempeleka mjomba wake kununua vitu Ocadeco
"Polisi waliniulizia, dada
yangu aliwauliza nyie ni kina nani, wakamueleza kuwa wao ni ndugu zetu, dada
yangu aliwaambia sisi hatua ndugu kama nyie", alieleza Masogange
Alieleza kuwa polisi hao
walimuweka chini ya ulinzi dada yake na kumtaka ampigie simu na ajifanye
anaumwa ili arudi nyumbani
Masogange alieleza kuwa dada yake
alimpigia simu na kumueleza anaumwa sana, naye akamjulisha kuwa ataenda muda
sio mrefu, lakini alikwenda saa 12 jioni
Alidai kuwa ilipofika nyumbani
kwake getini kabla hajashuka kwenye gari alimuona mlinzi amekaa na watu
wanne, aliwasalimia na kuingia ndani.
Aliendelea kudai kuwa ilipofika
ndani alimkuta dada yake, askari wa kike na askari wawili wa kiume,
walimueleza wanasubiri yeye na wakajitambulisha kuwa wao ni polisi.
Masogange alidai kuwa aliwauliza
wanashida gani na wakamueleza kuwa wamekwenda kufanya upekuzi, wakapekuwa
wakamueleza kuwa hawatapata kitu chochote.
Alidai baada ya upekuzi huo,
alichukuliwa na kupelekwa kituo kuu cha polisi na kwamba walipofika mapokezi
akaandikisha jina na wakampeleka rumande ambapo alikaa siku tisa.
Aliongeza kuwa baada ya kukamatwa
Februari 14, 2017 na Februari 15, 2017 akiwa polisi alipelekwa katika ofisi
iliyokuwa na watu 15 ambapo kwa nyakati tofauti alikuwa akimuuliza maswali.
Baada ya mahojiano, Masogange
alidai kuwa alipelekwa Mwananyamala ambapo alioneshwa picha mbili za wanaume
wawili, akaulizwa kama anawafahamu na kuwaeleza kuwa hawafahamu
Alidai baada ya hapo alipelekwa
kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo afande Judy alishuka katika gari
walilokuwa nalo, akamuita mama wa makamo, akamuomba kikontena kidogo cha
plastiki cha kuhifadhia mkojo na Masogange akaambiwa angozane na mama hiyo
Aliendelea kudai aliongozana naye,
wakaingia chooni ambapo huyi mama wa makamo alimkabidhi kikontena hicho cha
kuwekea mkojo, akaingia chooni mwenyewe akatoa mkojo na kumkabidhi hiyo mama
wa makamo .
Masogange alidai kuwa baada ya
hapo afande Judy walimueleza hiyo mama wa makamo kuwa watawasiliana, na
akarejeshwa polisi.
Masogange aliendelea kutoa utetezi
wake alidai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.
Alibainisha kuwa mtu anayetumia
dawa za kulevya hawezi kuhimili kukaa siku bila ya kutumia dawa za kulevya
utetemeka na kuwa kama amechanganyikiwa, lakini yeye alikaa na hali yake
ikiwamo nzuri
" Mheshimiwa mimi sijawahi
kutumia dawa za kulevya hata siku moja nipo tayari hata mahakama yako
ijiridhishe kwa kunipima." Alieleza Masogange
Wakili wa Serikali, Kakula
alimuuliza Masogange kuwa ni sahihi alikamatwa Februari 14,2017.
Masogange ni kweli
Kakula ni sahihi Februari 15,2018
ulipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Masogange: kweli Kakula
uliongozwa na askari wa kike akiwa na chupa
Masogange hapana
Kakula ni sahihi huo mkojo ni wewe
mwenyewe uliutoa na kumkabidhi yule mama wa makamo
Masogange: ndiyo
Masogange katika kesi hiyo
anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana
ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin
(Diacety Imophine
0 MAONI YAKO:
Post a Comment