February 15, 2018

Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba, amefunguka leo hii kuhusu ujio wa Wimbo mpya wa Papii kocha na Baba yake mzee nguza. Akizungumza na xxl ya CLouds Fm, ndugu Ruge pia amezungumzia kuhusu show ya jumamosi inayowahusisha wanamuziki Aslay na Nandy itakayofanyika Ascape One


 "Kuhusu show ya #MapenziMubashara18 Jumamosi. Ruge alisema kila kitu kinaend vizuri katika viwango vya kutisha na ana uhakika watakaohudhuria watasimulia milele."
 
Kuhusu tetesi kwamba #PapiiKocha na #BabuSeya watakuwa sehemu ya show ya Jumamosi Ruge alisema 
"Nadhani hayo tuyaache kwanza lakini habari kubwa ni kwamba kesho #PapiiKocha anatoa video".  
Ruge amesema Watanzania wakae tayari kwa kitu kikubwa, ikiwa ni wimbo wa kwanza baada ya Papii na Baba yake kukaa jela kwa miaka 14.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE