Kundi la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Sol limeungana na maelfu
ya Wakenya mtandaoni kupinga hatua ya serikali ya jiji la Nairobi
kuwakamata MaDeej’s wanaopiga muziki kuanzia saa sita usiku kwa madai
kuwa wanachafua mazingira kwa makelele.
Sauti Sol wamesema kuwa huwezi kukamilisha muziki katika klabu kama
hakutakuwa na DJ, Hakuna mtu mwingine atakayefanya sherehe yako inoge
kama hautakuwa na Dj na kutamka rasmi kuwa wanaungana na Wakenya wenzao
katika kutafuta haki juu ya ukamatwaji wa MaDJ’s ambao wanajitafutia
riziki kupitia mikono yao.
“As an artist, who do you turn to for support when you have
new content out? As a fan, who do you go to when you’re at a party,
event or in the club and want to request for your fav joint? The Dj!
Therefore, let’s all join the #StopArrestingDjs thread and show support for our DJs.“wameandika Sauti Sol kupitia ukurasa wao wa Twitter.
Maelfu ya Wakenya jana na leo wameanzisha mtandaoni Hashtag maalumu
ya #StopArrestingDJs kuishinikiza serikali na Gavana wa Jiji la Nairobi,
Miko Sonko kuwaachia maDJs wote waliokamatwa kuanzia wikiendi
iliyopita.
Kikosi hicho kinachowakamata MaDJs kinaongozwa na Jeshi la Polisi
kushirikiana na watu wa Mamlaka ya Mazingira nchini Kenya (NEMA) na
mpaka leo asubuhi Madeej’s wawili Riggz na Tremor pekee ndio walioachiwa
kwa dhamana huku wengine wakiwa bado wameshikiliwa.
Hata hivyo, Jana DJ maarufu nchini Kenya Creme del a creme alienda
hadi Kituo Kikubwa cha Polisi jijini Nairobi na kufanikiwa kuwatoa
Madeej’s wawili walioshikwa kutoka Alchemist club.
Watu wengi nchini Kenya wamelaumu hatua hivyo wakidai kuwa ni
unyanyasi huku wakitaka hatua hiyo ianzie kwa wamiliki wa Club na kumbi
za starehe na sio kuwakamata moja kwa moja Madeej’s.
Wasanii na watu maarufu nchini Kenya wameshaunga mkono kampeni hiyo mitandaoni kushinikiza Madeej’s wasikamatwe.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment