
Raia wa Pakistan Abdul Waheed mwanzoni mwa mwaka 2017 alifungua kesi mahakamani kushinikiza kufutwa kwa kusherehekewa kwa siku hiyo nchini Pakistani kwa madai kuwa siku hiyo inaeneza uasherati, uchafu na uovu nchini humo.
Februari 13, 2017 siku moja kabla ya Siku ya Wapendanao, Jaji Shaukat Siddiqui alitoa amri ya kupiga marufuku kabisa programu yoyote ya matangazo kuhusiana na siku hiyo pamoja na kuweka vikwazo vingine.
Kutokana na watu na mamlaka mbalimbali kutoa maoni yao kupinga suala hili, inatarajiwa kusherehekewa kwa siku hii pengine kukafutwa kabisa nchini humo. Maamuzi ya mwisho ya mahakama juu ya hatma ya siku hii bado yanasubiriwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment