Viongozi mbalimbali wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo wakikagua miundombinu iliyojengwa kwa shule ya msingi Kitongamango.

Madarasa mapya yaliyojengwa katika shule ya
msingi Kitongamango.

Wanafunzi wa Shule ya msingi Kitongamango
wakimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.

Jengo la Ofisi ya Walimu na madarasa katika shule
ya msingi Boga.

Majengo mapya ya Shule ya msingi Boga.
Wanafunzi wa shule za msingi Kitongamango na Boga wilayani
Kisarawe wameishukuru serikali kwa kuwajengea madarasa mapya, vyoo vya
kisasa pamoja na Ofisi za walimu za walimu katika shule zao.
Shukrani hizo wamezitoa kwa serikali wakati wa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani alipokuwa akizindua miundombinu hiyo katika
shule hizo.
Shule hizo pamoja na shule ya msingi Mitengwe zilikuwa katika
hali mbaya ya miundombinu hiyo lakini kwasasa zimejengewa na kuonekana za kisasa.
Miundombinu iliyojengwa ni pamoja na vyumba vya madarasa 4, vyoo
matundu 10, na Ofisi za walimu kwa kila shule, hali ambayo imebadili mazingira
ya shule hizo.
Kufuatia hali hiyo, Wanafunzi hao wamemshukuru Rais Dkt. John
Pombe Magufuli na Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo kwa kubadilisha shule
zao kwa kuweka mazingira mazuri ya kusomea.
Wamemuahidi Waziri Jafo kusoma kwa bidii katika na kufanya
vizuri kwenye masomo yao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment