
MWANAMAMA Leyla Mtumwa (36) mkazi wa
Arusha ameuawa jijini London nchini Uingereza kwa kuchomwa visu na
mwanaume mwenye umri wa miaka 38 (jina halijatajwa) anayedaiwa kuwa ni
mpenzi wake baada ya kutoka disco usiku wa kuamkia jana Machi 30, wote
hawa ni Raia wa Tanzania.Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kamkia jana Machi 30, 2018,
katika nyumba wanayoishi Watanzania hao iliyopo eneo
la Haringey, Kirkstall Avenue, N17 jijini London, baada ya kuzuka
ugomvi baina yao ikiwa ni muda mfupi baada Leyla kurejea nyumbani
akitokea disco la usiku alikokuwa amekwenda na marafiki zake.Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa, alirudi kutoka disco akiwa na rafiki
yake wamelewa na kuingia ndani, ambapo alimkuta mpenzi wake ambaye
alianza kufoka na kutukana jambo lililoibua mzozo mkali baina yao.

Baada ya mzozo huo kuwa mkubwa rafiki aliondoka na ndipo jamaa huyo
alianza kumshushia kipigo kisha kumchoma visu mbele ya mtoto wake wa
miaka 12, ambaye Leyla alizaa na mumewe wa kwanza anayedaiwa kuwa ni
raia wa Nigeria.

Ikiwa ni majira ya saa 1:00 asubuhi, hali ya Leyla ilikuwa mbaya, kijana
huyo alipiga simu katika kitengo maalum cha polisi cha makosa ya jinai
(Met’s Homicide and Major Crime Command), kuwajulisha tukio hilo .Kwa mujibu wa Met’s Homicide and Major Crime Command, baada ya polisi
kuwasili walimkuta Leyla akiugulia majeraha ya visu huku akilia maumivu
makali aliyokuwa akiyapata, walimchukua kwa Ambulance na kumpeleka
hospitali.Licha ya jitihada za polisi kuwahi, lakini Leyla aliaga dunia majira ya saa 2:11 asubuhi kwa saa za London. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku wakimshikilia mwanaume huyo wa Leyla kama mtuhumiwa namba moja wa tukio hilo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment