Nyota ya mchezaji kutoka Tanzania Shiza Kichuya inatarajiwa kung’aa
zaidi. Amepata mwaliko wa kujiunga na vigogo wa Ujerumani Bayern Munich
kusakata soka katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.
Kocha Juup Heynckes amemsifu mchezaji huyo matata wa klabu ya Simba S.C, kuwa na uweledi, chenga, pasi za uhakika, mwendo wa kasi na kismati ya kufunga mabao. Mambo ambayo yamemvutia kumsajili katika kikosi chake. Katika mahojiano na DW, mshambuliaji wa Bayern Arjen Robben amesema anasubiri kwa hamu kuu kufanya mazoezi ya kwanza na Kichuya. Usajili wa Kichuya utaigharimu Bayern euro milioni tano.

Akihojiwa na DW, Kichuya amesema ndoto
yake ya kucheza miongoni mwa wachezaji bora duniani kama Arjen Robben,
Robert Lewandowski na Franck Ribery imetimia. Kichuya anatarajiwa
kuwasili katika uwanja wa Allianz Arena jijini Munich msimu ujao.
-
Ikiwa umeiamini taarifa hii, basi tumefaulu kukufanyia utani siku hii ya kutaniana (April Fools' Day). (Kwa Kichuya; kikosi cha #DWKiswahili kinaamini kuwa uchezaji wako ni wa hali ya juu kukuwezesha kuvichezea vilabu vikubwa vya ligi zinazosifika duniani. Lakini kwa leo ni matani-#AprilFools'Day!)

0 MAONI YAKO:
Post a Comment