April 11, 2018

 
Klabu ya Liverpool imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuifunga Manchester City kwa jumla ya mabao 5 – 1.Liverpool inafanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kupita miaka 10 bila kufanya hivyo wakati kwenye mchezo wake wa hapo jana timu hiyo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya Manchester City.
Takwimu zinaonyesha kuwa Liverpool imefika hatua ya nusu fainali ya michuano ya European Cup/Champions League mara 10 kwa timu za Uingereza huku kinara ikiwa ni Man United ambayo imeingia mara 12.
Huku historia ya Liverpool inaonyesha kuwa Roberto Firmino na Mohamed Salah wamefunga zaidi ya mabao nane kwenye kila mashindano ya Champions League na European Cup kuliko wachezaji wowote ndani ya klabu hiyo.
Man City: Ederson (6), Walker (6), Otamendi 6), Laporte (5), Bernardo Silva (7), Fernandinho (7), De Bruyne (7), David Silva (6), Sterling (7), Gabriel Jesus (6), Sane (7).
Wachezaji waakiba: Gundogan (6), Aguero (6).
Liverpool: Karius (6), Alexander-Arnold (7), Lovren (7), van Dijk (6), Robertson (6), Oxlade-Chamberlain (6), Wijnaldum (6), Milner (8), Salah (7), Firmino (7), Mane (6).
Wachezaji waakiba: Clyne (6), Klavan (6), Ings (N/A)
Mchezaji bora wa mchezo huo: James Milner

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE