
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
ameweka wazi kuwa hatua inazopiga serikali kudhibiti uchumi, waliokuwa
na tabia za kutuibia rasilimali hawawezi kufurahia, hivyo watatumia njia
yoyote kukwamisha ikiwemo kuchonganisha.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akihutubia umma wakati wa
uzinduzi wa ukuta uliojengwa kuzunguka eneo lenye madini ya Tanzanite,
ambayo yanapatikana Tanzania pekee .
Rais Magufuli amesema watu hao wakiwemo wale waliokuwa wanaiba
wanyama na kuwasafirisha kwa ndege ili miaka ya baadaye wasiwe na sababu
ya kuja Tanzania kutalii, watatumia mbinu yoyote kuhakikisha Tanzania
haifanikiwi kujikwamua kiuchumi, ili waje watawale tena.
“Awamu ya tano inapambana vita ya uchumi, vita ya uchumi
ni ngumu, inapambana na mabeberu ya kila aina, tunaowazuia wizi hawawezi
wakafurahi, tunapowazuia wizi wa dhahabu hawawezi wakafurahi, waliokuwa
wanasafirisha wanyama wetu kwenye ndege wakiwa hai ili miaka ijayo
wasije hapa kutalii, hawawezi wakafurahi. Na ni watu wenye uwezo mkubwa,
mengine ni mataifa makubwa kutoka nje, wataleta vitimbwi vya kila aina,
watawachonganisha kwa kila aina, kwa sababu ukitaka watu uwatawale ni
kuwachonganisha”, amesema Rais Magufuli.Rais Magufuli ameendelea kwa kusema ...”wapo waliokuwa wanataka nchi yetu isiendelee, unanunua ndege, wanatumiwa watu wanashangilia kukamatwa ndege yao, ni ushetani kweli kweli, ndege ni yenu, mtapanda wote lakini mtu anasimama pale anasema afadhali imeshikwa, ibaki huko huko, mnajiulizaje mtu wa aina hiyo, mali ni yenu, imeshikwa ni mali yenu lakini wanashangilia.
Sambamba na hilo Rais Magufuli amewataka watanzania kuwa wazalendo na kuzingatia uchumi wa nchi, na sio kushangilia pale panapotokea tatizo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment