
Dkt. Magufuli amesema hayo leo Alhamisi, Aprili 26, 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Lengo la Serikali yetu kuhamia Dodoma lipo palepale, hatuwezi kurudi nyuma. Sasa hivi zaidi ya watumishi 3,800 wameshahamia, mimi nitahamia Dodoma mwaka huu. Dodoma ndiyo Makao Makuu. Kwa mamlaka mliyonipa, natangaza rasmi kuanzia leo Aprili 26, 2018, Manispaa ya Dodoma itakuwa Jiji la Dodoma, mkurugenzi wake ataanza kuitwa Mkurugenzi wa Jiji“, amesema Dkt. Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amesema maandalizi yote ya kisheria yaanze kutumika katika jiji hilo jipya ambalo litakuwa Jiji la kipekee kwa sababu lipo katikati ya Tanzania.
Sasa Tanzania inakuiwa na jumla ya majiji sita , mengine ni
Dar es Salaam,
Tanga,
Arusha,
Mbeya,
Mwanza
0 MAONI YAKO:
Post a Comment