Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu tisa
waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue Posta, Dar es Salaam.Kamanda wa Polisi Kanda, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa
watu hao. Kukamatwa kwao kumekuja mara baada ya Jeshi la Polisi kuonya
kuwa litawachukulia hatua kali wale wote watakaokaidi agizo la
kutoandamana kama walivyoagiza.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia kwa
mahojiano Diwani wa Kata ya Igumbiro, Musa Mlawa kwa kosa la kufanya
mkusanyiko usio halali.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire Diwani
huyo anashikiliwa kwa mahojiano ili kubaini chanzo cha mkusanyiko huo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment