
Aliyewahi kuwa mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia
alikuwa Mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph
amefunguka na kusema kuwa hazitapita siku tatu lazima alipue bomu.
Mzee
Yussuf amesema hayo baada ya moja ya mtu ambaye alifahamiana naye kwa
masuala ya kidini lakini baadae amekuja kumbadilikia jambo ambalo
amesema sasa limempa mafunzo ila lazima aliweke sawa ndani ya siku tatu
hizi.
Baada ya kauli hiyo watu wengi walianza kumpa pole Mzee Yussuf huku wengine wakitamani kujua jambo gani ambalo limempata mpaka kutoa kauli kama hiyo ambayo inaonyesha wazi kabisa kuwa kuna jambo halipo sawa, ndipo hapo aliposema kuwa lazima aliweke sawa jambo hilo ndani ya siku tatu hizi.
"Mtanielewa tu Insha Allah ngoja bomu lilipuke, labda Allah aniokoe lakini siku hizi tatu kutoka leo hesabu tu lazima niweke wazi" alisema Mzee Yussuf
0 MAONI YAKO:
Post a Comment