August 07, 2018

Image result for rostam 

Baada ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kudai kwamba Roma Mkatoliki na Stamina hawakuitwa na baraza hilo kwaajili ya wimbo wao mpya ‘Parapanda’ na kudaiwa wanatafuta kiki, Stamina ameamua kuweka wazi kila kitu baada ya sakata hilo kuonekana kuchukua sura mpya.
Rapa huyo amedai wao hawatafuti kiki kama baraza lilivyodai na kudai kwamba wanalishukuru baraza hilo kwa kutangaza kwa wimbo wao haujafungiwa.
“Sisi kama ROSTAM tunaamini kile tunachokifanya na hatujawahi kufanya muziki kwa mlengo huo wa kiki. Mwenye uelewa ukisoma hiyo barua utaelewa kama tunatafuta kiki au kweli tuliitwa kwa ajili ya wimbo wa Parapand,” alisema Stamina kupitia taarifa yake aliyoitoa mtandaoni.
             

Aliongeza, “Hata hvyo tunawashukuru BASATA kwa kuthibitisha mbele ya umma leo kua nyimbo haijafungiwa. Pia Tunashukuru mashabiki kwa kuendelea kusupport muziki wetu, naomba tuendelee kuuchagua wimbo wetu kwenye media mbalimbali #Hatuongeitena #achagomaliendelee. Asante,”
Basata mapema leo waliiambia Bongo5 kwamba hawajaufungia wimbo Parapanda na wanashangaa kwanini wasanii hao waliamua kusambaza taarifa hizo.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE