Kocha maarufu mkoani Morogoro na mwalimu wa timu ya Black Viba ya ligi daraja la tatu manispaa ya
Morogoro, Kibwana Ally "Gebo", amefariki dunia. Teacher Gebo amefariki ghafla asubuhi ya leo
baada ya kusumbuliwa na presha ya kushuka . Taarifa
zilizofika
na kuthibitishwa na katibu mkuu wa chama cha soka wilaya ya Morogoro
mjini "MMFA", Bwana Kafale Maharagande, zinasema kuwa "Gebo" amepatwa na
umauti asubuhi ya leo na mipango ya mazishi inaendelea huku marehemu
akitarajiwa kuzikwa siku ya kesho jumatatu. "Mie jana nilionana nae
akiwa mzima kabisa na tumeongea kidogo. Maana aliniletea ratiba.
Kiukweli ni pigo katika soka la manispaa, kwakuwa Gebo ni mtu ambaye
alikuwa ana hamasisha mchezo wa soka kupitia timu yake ya muda mrefu ya
Black Viba." Alisema Maharagande.
Taarifa hii imekuwa ni pigo kwa timu ya Black Viba ambayo kesho inatarajia kucheza mchezo wa sita bora wa ligi daraja la tatu dhidi ya majirani zao Kaizer Chief Fc (Manzese).
(Haijathibitishwa kama mchezo huo utasogezwa mbele ama laah, japo kuna uwezekano mkubwa wa kufanya hivyo). Wakati wa uhai wake Gebo aliwahi pia kuwa mchezaji mahiri wa vilabu kadhaa ndani ya Manispaa ya Morogoro kama BLACK VIBA, FRUITS FC, SOKO KUU, BARCELONA FC(BOMA ROAD), MAZAO FC ambayo sasa MZINGA, MNADANI FC, UHURU RANGERS, na SULTAN RANGERS.
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahala pema peponi.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment