October 28, 2018

Frenkie de Jong 
Manchester City huenda wakawapiku Tottenham katika kumwinda kiuungo wa kati wa Ajax Frenkie de Jong, 21. (Daily Star Sunday)
Meneja wa zamani wa Chelsea manager Antonio Conte na kocha wa Juventus Max Allegri wametajwa kuwa wale wanaweza kuchukua nafasi yake Jose Mourinho kama meneja wa Manchester United mwaka ujao. (Sunday Express)

Juan Mata 
Arsenal watajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Juan Mata ikiwa Mhispania huyo mwenye miaka 30 ataondoka bila mkataba msimu ujao. (Daily Star Sunday)


Paul Pogba
Juventus wanataka kumrudisha Paul Pogba kwenye klabu na watatoa ofa kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25 kiungo wa kati wa Manchester United mwezi January. (Tuttosport, via Mail on Sunday) 

Manchester United wamemuamrisha Pogba aache kuzungumzia matatizo yake na meneja Jose Mourinho na uwezekano wake wa kuondoka Old Trafford. (Sunday Mirror)Manchester United wamemuamrisha Pogba aache kuzungumzia matatizo yake na meneja Jose Mourinho na uwezekano wake wa kuondoka Old Trafford. (Sunday Mirror)
 Miguel Almiron 
West Ham wanatarajiwa kujiunga katika mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Atlanta United Miguel Almiron, mchezaji mwenye miaka 24 raia wa Paraguay kwa pauni milioni 25. (Football.London)

Malcom 
 
Tottenham imepanga kumsainisha mchezaji wa Brazil Malcom, 21,wa Barcelona ambaye anahangaikia kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho na Ousmane Dembele. (Corriere dello Sport - in Spanish)

Kiungo wa kati Mousa Dembele, 31 yuko katika orodha ya juu ya wachezaji wa Tottenham ambao meneja Mauricio Pochettino anataka kuwauza katika kipindi hiki cha kiangazi. (Sun)
Kiungo Aaron Ramsey, 27,amejihudhuru ili aondoke timu ya Arsenal katika kipindi cha kiangazi, ingawa amesema kuwa anashangaa kwanini Arsenal wamesitisha tena mkataba wake wa miaka minne (Evening Standard)

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE