Mtandao wa kijamii wa Facebook kwa sasa inakumbwa na hali mbaya zaidi
ya mawasiliano kuwahi kutokea katika historia yake kwani huduma nyingi
hazipatikani kote ulimwenguni. “Tunafahamu kuwa baadhi ya watu hawana
hawawezi kufikia app zinazohusiana na Facebook ,” ilisema taarifa
iliyotolewa na Facebook.
Haijabainika
wazi ni nini kinachosababisha shida hiyo. “Tunafanya kila juhudi
kushughulikia tatizo lililopo haraka iwezekanavyo.” Kando na Facebook yenyewe, huduma za Messenger na Instagram zimetatizwa. Mara
ya mwisho Facebook ilijipata katika hali hiyo ilikuwa mwaka 2008 wakati
mtandao huo ulikuwa na watumiaji milioni 150 -ikilinganishwa na sasa
ambapo watumiaji karibu wanakadiriwa kuwa karibu bilioni 2.3 kwa mwezi. Kampuni
ya Facebook imejibu uvumi unaoendelea mitandaoni kuwa huenda mtandao
huo maarufu duniani umedukuliwa. Inasema hali hiyo haijatokana na
shambulio lolote la kimtandao
Tatizo ni kubwa kiasi gani? Inakadiriwa
kuwa tatizo hilo lilianza kukumba mtandao huo siku ya Jumatano. Japo
huduma ya Facebook ilionekana kuwa sawa watumiaji wake waliripoti kuwa
na hawawezi kutuma ujumbe. Watumiaji wa Instagram hawawezi kufikia
ujumbe mpya huku wale wanaotumia huduma ya Facebook Messenger kupitia
kompyuta pia wakikabiliwa na changamoto sawia na hiyo. Hata hivyo
watumiaji wa mtandao huo kuptia app ya simu waliweza kutuma baadhi ya
ujumbe japo nao pia walielezea kupata changamoto ya kutuma picha.
Mtandao wa WhatsApp, pia uliathiriwa na changamoto hizo. Hali hiyo imeathiri kampuni zinazotumia Facebook kuendesha biashara zao kwasababu walishindwa kabisa kuwasiliana.
Mwana
mitindo Rebecca Brooker ambaye anatumia mtandao huo kufanya kazi yake
mjini Buenos Aires ameiambia BBC kuwa hali hiyo imeathiri pakubwa
biashara yake. “Facebook kwa matumizi ya kibinafsi ni sawa lakini
kwa kampuni kubwa zinazoendesha huduma zao kupitia mtandao huo
unatarajia hii inamaanisha nini kwao?” alisema. Nchini Uingereza mshauri
n a mtaalamu wa magonjwa ya watoto aliiambia BBC kuwa wafanyikazi
wenzake walisikitika na kukatizwa kwa huduma hizo kwa sababu walikuwa na
hafla ya kumuaga muuguzi mmoja ambaye amehudumu kwa miaka 20. “Ilikuwa
siku ya kazi na washauri wengi hawakuweza kufika lakini walitegemea
kutumia whatsApp kujumuika pamoja,” alisema Dr Nikhil Ganjoo. “Kwa hivyo
nililazimika kuwaakilisha lakini sikuweza hata kuwatumia picha za
matukio katika hafla hiyo.”
Tatizo
hilo linatokea wakati wabunge nchini Marekani wanatafakari uwezekano wa
kuvunjilia mbali makampuni makubwa ya teknolojia – si tu Facebook.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment