April 23, 2019

 Diva Giving For Charity ni project maalum ya kuchangia watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi iliyoanzishwa na mtangazaji maarufu wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds fm Diva Loveness Love maarufu @Divatheebawse. Project hii inatakliban miaka mitano sasa tangu kuanzishwa kwake na kwa kipindi chote ilikuwa ikifanyika Jijini Dar Es Salaam pekee.
 

Mwaka huu wa 2019 Diva aliamua kuvuka mipaka na kutoka nje ya Dar es salaam na kufika mkoani morogoro katika Kituo cha Raya  Islamic Orpharnage Centre katika kijiji cha Mindu nje kidogo ya mji wa Morogoro. Katika tukio hilo lililofanyika siku ya Pasaka, mtangazaji Diva aliwakilishwa na mwanamuziki WHOZU , huku mkurugenzi wa Samaki Spot Farida Mees na kampuni ya Beeer Oclock wakiwa kipaumbele katika kufanikisha hilo. Katika tukio hilo pia wasanii toka mkoani Morogoro Mycoely, strevol na producer toka kwanza Records Vennt Skillz wakisimama mstari wa mbele kabisa.Lakini Pia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiislam mkoani Morogoro MUM wanaochukua Diploma ya Maabara waliungana na timu hii ya Diva katika kufanikisha hilo.   Miungoni mwa vitu vilivyokabidhiwa na timu hiyo ni pamoja na Unga, mchele, mafuta, Sabuni, kitanda nk,




 Baadhi ya vifaa hivyo.






 Mwanamuziki WHOZU akiskiliza Kero kwa umakini


Picha zote zimepigwa na Drama Studio TZ

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE