Pazia la kumsaka Miss Marogoro wa mwaka 2019 - 2020 , limefunguliwa Rasmi katika ukumbi wa Thedome pale Samaki Spot. jumra ya washiriki 8 kati ya 12 walijitokeza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kuelekea katika fainali za kumpata mlimbwende huyo atakayeondoka na zawadi Kabambe chini ya waandaaji Nyumbani Park .
Washiriki wakijitambulisha mbele ya wageni waalikwa |
Akizungumza katika uzinduzi huwo, afisa habari wa Miss Morogoro Warda Makongwa, amewaomba wadau na wadhamini kushirikiana pamoja katika kuhakikisha Morogoro inampata mshiriki mwenye vigezo atakayeweza pia kuuwakilisha vema mkoa wa Morogoro katika Kilele cha Miss Tanzania 2019.
Mwendesha shughuli pia MC Maarufu nchini MC Kondo, amehakikisha kwamba kama tutashirikiana kwa pamoja , basi tuna hakika mshindi wa Miss Tanzania 2019 atatoka katika mkoa wa Morogoro na itakuwa historia kwa mara ya kwanza kwani Mkoa wa Morogoro haujawahi kutoa mshindio wa Taji hilo tangu kurejeshwa kwa mashindano hayo mwaka 1994.
wageni waalikwa wakifwatilia kwa umakini uzinduzi
MC Warda Makongwa ambaye pia ni afisa habari wa Miss Moro akihakikisha mambo yanakwena sawasawa
MC Kondo na MC Warda Makongwa
Mmoja ya wadhamini Nuba akifwatilia kwa makini
DJ maarufu Moro DJ Fradoh akiwa na MC Kondo wakiteta jambo
Mkurugenzi wa Miss Morogoro Farida Kulususu akiongea jambo japo hakuwa powa kiafya lakini alihakikisha mambo yanakwenda sawa sawa
Barnaba akicheza na mmoja ya mashabiki wake
Barnba Classic akiwaburudisha wageni waalikwa
Kilele cha mashindano hayo ya Miss Morogoro 2019 kinatarajiwa kufanyika siku ya 22 June 2019 Jumamosi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment