April 28, 2019

 

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz, amethibitisha kurejea hospitalini nchini  Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu awali kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake (Checkup).


Ommy Dimpoz amethibitisha hilo, kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema anamshukuru Mungu kwani uchunguzi huo umekwenda salama kwa kuandika ”Alhamdulilaah Mungu Ni Mwema”.
Ommy Dimpoz amerudi Ujerumani ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu afanyiwe upasuaji wa koo mwishoni mwa mwaka jana.
Hii inaweza kuwa ni habari nzuri kwa mashabiki wake kwani ameonesha kuwa kwa sasa afya yake iko poa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE