April 26, 2019




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewaondoa kwenye orodha ya waamuzi wa msimu huu, Abdallah Kambuzi, Godfrey Msakila na Consolata Lazaro waliochezesha mchezo kati ya KMC na Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jana Aprili 25, 2019.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na shirikisho hilo, waamuzi hao wameondolewa kuchezesha mechi zilizosalia za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha kwenye mchezo huo.
Katika mchezo huo Kambuzi alikuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Godfrey Msakila na mwamuzi msaidizi namba mbili Consolata Lazaro.
Katika taarifa hiyo, TFF imewaonya waamuzi wote wa ligi kuu, ligi daraja la kwanza na daraja la pili kuwa makini
“Yeyote atakayebainika kuchezesha chini ya kiwango kwa namna yoyote atakuliwa hatua stahiki”, imeeleza taarifa hiyo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE