Rais Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,530 ambapo wafungwa 722 wataachiliwa huru siku ya leo April 26, 2019.
Taarifa
iliyotolewa na Meja Jenerali Jacob G Kingu, imeeleza kwamba wafungwa
2808 watabaki gerezani kumalizia kifungo kilichobaki baada ya kupewa
msamaha huo.
Wafungwa
wengine waliobahatika msamaha huo ni pamoja na na wale wanaougua
magonjwa kama Ukimwi, Kansa na Kifua kikuu ambapo watathibitishwa na
Jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu Mkoa au Wilaya.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment