
Klabu ya Azam imefuzu hatua ya pili
ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya
Fasil Kenema ya Ethiopia katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi
Complex, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Richard Djodi, aliyefunga mabao mawili
katika dakika za 23 na 31 na Chirwa akafunga bao la tatu dakika ya 59
wakati bao la Kenema likifungwa na Mujib Kassim dakika ya 37. Azam
wanafuzu round ya pili kwa Agg 3-2 baada ya mchezo wa kwanza nchini
Ethiopia kufungwa bao 1-0.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment