Na. Luppy Kung’alo, Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel s/o Lusega miaka (42) kabila mkaguru na mkazi wa Morisheni kata, tarafa na wilaya ya kongwa kwa tuhuma za kumchinja mke wake na kumuua.
mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel s/o Lusega miaka (42) kabila mkaguru na mkazi wa Morisheni kata, tarafa na wilaya ya kongwa kwa tuhuma za kumchinja mke wake na kumuua.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la
Polisi Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema Tukio hilo limetokea tarehe
25/06/2012 muda (08:00hrs) wa saa mbili asubuhi leo, katika eneo la
Morisheni Kata, Tarafa na Wilaya ya Kongwa.
“Mtuhumiwa
alikwenda kuripoti mwenyewe katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya
Kongwa kuwa amemchinja na kumuua mke wake kwa sababu hamsikilizi.”
alieleza Kamanda Zelothe.
Bw,
Zelothe alisema mtuhumiwa huyo wakati anaripoti tukio hilo katika kituo
cha Polisi alikuwa na barua mkononi ikieleza madai hayo kwa marehemu
mke wake, ikiwa na anuani ikielekeza kwa Afisa Usalama wa wilaya ya
Kongwa, lakini barua hiyo ameikabidhi katika kituo cha Polisi.
Kamanda
ZELOTHE STEPHEN alimtaja mwanamke huyo aliyeuwawa kuwa ni Telophena w/o
Machimo umri miaka (34) kabila Mkaguru, muuza mgahawa na Mkazi wa
Morisheni wilayani kongwa.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema
askari walikwenda kukagua eneo la tukio na kukuta marehemu amechinjwa
kwa kukatwa koromeo na akiwa katika dimbwi la damu
pamoja na kisu kilichotumika kikiwa kando yake.
pamoja na kisu kilichotumika kikiwa kando yake.
Alisema
chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwa kuwa mtuhumiwa alikuwa
akimtuhumu marehemu kwa kutembea nje ya ndoa pia kwa kutoleta matumizi
ili hali merehemu ni muuza mgahawa katika eneo hilo.
Hata hivyo Kamanda Zelothe
alisema mtuhumiwa huyo ana historia ya ugonjwa wa akili kwa mujibu wa maelezo ya wanandugu na viongozi wa kijiji wa eneo hilo.
"Mtuhumiwa amekamatwa na anashikiliwa katika kituo cha Polisi Wilayani Kongwa na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo
mkabili" alisema Bw. Zelothe.
mkabili" alisema Bw. Zelothe.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment