Baada
ya mapokezi hayo millardayo.com ilipata nafasi ya kuzungumza Exclusive
na Dogo Janja ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi na kusisitiza
kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi
kwamba zile zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu
ambacho amekikubali kwa roho safi.
Janja
amesema bado hajasaini mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu
wake wawili anaowasubiri kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba,
baada ya hapo ndio atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza.
Amesema
amebadili mawazo na sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri
ambayo aliahidiwa na Ostaz Juma meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa
shule na kurudishwa nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni kusoma
kwenye shule binafsi nzuri na pia swala lake la muziki kuzingatiwa.
kwenye
sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na
kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati”
Kwa
kumalizia Janja amesema kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli
mbiu ya wakati nilivyokujaga nilisema nawakalisha matembo sasa hivi
nawalaza chali matembo”
KWA HISSANI YA MILLAR AYO
0 MAONI YAKO:
Post a Comment