June 17, 2016

150726131608_caf_logo__512x288_nocredit_nocredit
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limepitisha majina ya wachezaji wanne wapya wa Yanga, kipa Benno David Kakolanya, Hassan Hamisi Ramadhan ‘Kessy’, Vincent Andrew Chikupe na Juma Hassan Mahadhi kucheza Kombe la Shirikisho.
Wachezaji hao wamesajiliwa kwa lengo la kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kimeingia kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho na wanatarajiwa kuanza kukipiga kwenye mechi ya kwanza ya kundi A dhidi ya Mo Bejala itakayopigwa nchini Afrika Kusini.
Yanga kwa sasa wameweka kambi nchini Uturuki pamoja na nyota hao wanne wakiwa tayari wameshaingia kwenye mipango ya Kocha Mkuu Mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiwa na Juma Mwambusi

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE