September 01, 2012

Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoriki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
 Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
 Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
 Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
 Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma. 
 Kati ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya Karume mjini Musoma. 
 Ray na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
Rais wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Profesa Jay akionesha uwezo wake wa kukamua jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mwasiti akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.
Mmoja wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super Nyota 2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Dimpoz na wanenguaji wake, wakiwajibika kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya viwanja vya Karume mjini Musoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Rachel (kushoto), akionyesha uwezo wake katika uwanja wa Karume mjini Musoma, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 na wanenguaji wake.
Rachel akikamua kwenye uwanja vya Karume mjini Musoma ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Msanii wa michano ya Bongo Fleva, Nay wa Mitego akipagawisha jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.

Related Posts:

  • Bernard Membe apata udhamini wa kishindo katika mkoa wa Ruvuma Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akilakiwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana, waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa mj… Read More
  • Mr. Nice amshukia Rais Mr. Nice Mr Nice amechukizwa na hatua za rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ya kutangaza nia ya kuombea urais kwa awamu ya tatu kinyume na katiba hali ambayo imesababisha machafuko. Rais wa Burundi Pi… Read More
  • Yasome maneno ya Ramadhan Singano baada ya mikataba yote kufutwa Simba SHIRIKISHO la soka TanzaniaTFF limezitaka klabu kushirikiana na SPUTANZA pamoja na Bodi ya Ligi katika kuweka mifumo mizuri ya uingiaji mikataba.   TFF inao mkataba mama (template) ambao klabu zote na wachez… Read More
  • Abou Diaby atemwa Arsenal   Mabingwa wa Kombe la FA mara mbili mfululizo Arsenal wamemtema kiungo wao Abou Diaby. Mchezaji huyo mwenye kipaji, 29, alikuwa akifananishwa na gwiji wa Arsenal Patrick Viera na kocha Arsene Wenger, lakini amekuwa … Read More
  • Ben Pol nitafunga ndoa ya kimila    Staa wa Bongo Fleva anaye fanya vizuri kwa sasa na ngoma yake ya ‘Sophia’ Ben Pol amefunguka kuwa atafunga ndoa ya kimila kwenye harusi yake. Akipiga stori na Clouds Fm hivi karibuni,alisema kuwa atafunga n… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE