
Bi. Kidude anaumwa na amelazwa katika hospitali ya
Hindu Mandal jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu wodi namba 202
kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na matatizo ya mapafu kwa
ajili ya moshi wa sigara.
Tukizungumza
na mmoja wa wanafamilia anayemuuguza leo hii Bi, Zainab Hussein amesema
leo ni siku ya tatu tangu kulazwa kwa Bibi huyo na kwa jinsi
tulivyomuona sisi hali yake inaendelea vizuri.
Hata hivyo hatukuweza kupata picha yake nzuri kutokana na msimamo wa familia ambao wamekataza mahojiano na kumpiga picha.
Leo asubuhi zilisambaa taarifa kwa BIBI KIDUDEamefariki Dunia habari ambazo si za kweli.
Tunamuomba mungu ampe afya njema ili aweze kulejea katika hali yake.
Picha kwa hissani ya www.dewji.blogspot.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment