November 02, 2012


                             Pasha, Diamond Na H Baba

Baada ya ngoma ya Diamond kuachiwa muda mfupi tu baadae nyimbo hiyo imeleta utata mkubwa kutoka kwa wasanii wawili tofauti ikishutumiwa kuwa ni idea ya wimbo wa Pasha aliomshirikisha Tunda Man upande wa beats na jina la wimbo ni H Baba kwa upande mwingine.
Wakizungumza na kituo cha Clouds Fm kupitia segment ya 255 ya kipindi cha XXl Pasha anasema alipigiwa simu na mshikaji wake akiambiwa kuhusu kufanana kwa nyimbo hizo na kwamba yeye pasha anasema alirekodi mwanzoni mwa mwaka huu na kwamba beat iliyotumika inafanana kwa asilimia 100 na nyimbo yake, wakati H Baba yeye anasema jina la wimbo huo ni kama jina la wimbo wake.
Akiongea  H Baba alikwenda mbali na kusema yeye alikuwa studio na KGT akirekodi wimbo wake aliomshirikisha Q Chief ndipo Diamond naye alifika hapo studio akiwa anaenda kufanya chorus ya nyimbo ya Shetta inayoitwa Nidanganye.
Anasema baada ya kuingia studio na kuwakuta wao yaani H Baba na Q chief Diamond aliusikia wimbo huo na kumwambia kuwa ameufagilia na kuwapa big up kwa kazi nzuri lakini anasema cha ajabu ameshangaa jana anaambiwa kuna wimbo unaitwa Nataka Kulewa na alipokwenda kucheki kwenye net akakuta ni kweli Diamond ameachia wimbo wenje jina hilo.
Akiongea kwa uchungu kupitia simu H baba amesema ameibiwa wimbo wake na Diamond ingawaje kwa kusikiliza wimbo wa Pasha upande wa beat na melodi hali inaonekana ni tet.
Swali la kujiuliza nani kati ya hao wawili Pasha na H Baba nani ameibiwa zaidi?

Related Posts:

  • Bodaboda wezi wa simu, wakamatwa na kuchomewa pikipiki   Maeneo karibu na Ocean Road, vijana maarufu kwa ukwapuaji wa simu za mkononi wakiwa kwenye pikipiki walimkwapulia dada mmoja simu. tukio hilo lilionwa na mtu aliyekuwa kwenye gari ndipo alipoanza kuwafukuzia na k… Read More
  • CUF- Wampeleka Lipumba UKAWACUF kimesema kimepanga kulipeleka jina la Profesa Ibrahimu Lipumba ili kuomba ridhaa ya kugombea kiti cha urais. Naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha wananchi CUF Bwana Shaweji Mketo amesema chama cha wananchi CUF kimepa… Read More
  • Mkurugenzi TPA asimamishwa kazi Waziri wa Usafirishaji Samweli Sitta.  Taarigfa zilizotufiki punde zinasema kuwa Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta amsimamisha kazi kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Bandari Tanzania mhandisi Madeni Kipande kutok… Read More
  • Runinga zilizojizima kupigwa fainiMamlaka ya mawasiliano nchini Kenya sasa inasema kuwa itavipiga faini vituo vya uninga vya NTV,KTN,Citizen na QTV nchini Kenya kwa kuzima matangazo yao kufuatia hatua ya serikali kuhamia katika matangazo ya dijitali. Mkurugen… Read More
  • Waliowajeruhi polisi Tanga wasakwaJeshi la Polisi nchini  limesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari sita kwa risasi mkoani Tanga. Askari hao walijeruhiwa wakati wakifanya kazi ya kuwatafuta watuhumiwa wa uhalifu wa kutumia silaha wanaodaiwa kuw… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE