February 15, 2015

CUF kimesema kimepanga kulipeleka jina la Profesa Ibrahimu Lipumba ili kuomba ridhaa ya kugombea kiti cha urais.
Naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha wananchi CUF Bwana Shaweji Mketo amesema chama cha wananchi CUF kimepanga kulipeleka jina la mwenyekiti wa CUF taifa Profesa Ibrahimu Lipumba katika umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA- ili kuomba ridhaa ya kugombea kiti cha urais dhidi ya majina yatakayoletwa na wagombea wa vyama vingine vinavyounda umoja huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu tarehe za kuchukua fomu kwa wagombea wa udiwani, ubunge na kiti cha urais, Bwana Mketo amesema kwa mujibu wa makubaliano na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi kila chama kitateua mgombea katika nafasi zote na kisha kushindanisha ili kupata mgombea moja atakayeungwa mkono na vyama vyote.
 

Aidha amesema katika nafasi ya viti vya udiwani na ubunge kwa wanaotaka kugombea fomu zitaanza kutolewa kuanzia machi 1 hadi 10 kupitia makatibu wa matawi na katika nafasi ya ubunge wagombea watatakiwa kuchukua fomu kwa makatibu kata na kuzirudisha kwa makatibu wa wilaya ambapo amesema aprili 17 hadi 19 kurugenzi ya uchaguzi inatarajia kukaa na kufanya mchujo kwa wagombea ubunge

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE