January 05, 2014


 Mbunge wa Kigoma kaskazini CHADEMA Zitto Kabwe Zuberi, amesema mbunge mwezie wa Chadema na mwanasheria wa hama Tundu Lissu, amemtuhumu kwamba amehongwa magari.
   Katikaukurasa wa Facebook Zitto ameandika madai hayo huku akitoa ufafanuzi juu ya magari aliyo nayo.

 "Wakili Tundu Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari moja mbili, freelnder ninayotumia Dar Es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni. Tuhuma hii haimo katika tuhuma nilizotuhumiwa nazo na kuandikiwa na chama ili kujibu. Kama Tundu lissu anadhani tuhuma hii ana ushahidi nayo wa kutosha aiongeze kwenye tuhuma walizoniandikia ili niweze kujitetea kwenye vikao, vinginevyo ni mipasho tu. Nawapa changamoto Tundu lissu na wenzake kama wana tuhuma Mpya dhidi yangu waniandikie kwa mujibu wa taratibu. Tuhuma nilizo nazo hivi sasa na ambazo nimezikatia rufaa katika Baraza Kuu zinahusu mkakati wa kugombea uenyekiti Taifa na kutaka mahesabu ya chama yakaguliwe na CAG".

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE