
“Sijaelewa damond kupata tuzo 7 alafu produza wake kutoka na 0!!!!!” ni jibu la moja ya maswali kuhusiana na tuzo hizo aliyokutana nayo Master J Jana alipokuwa mgeni katika session ya ‘Kikaangoni Live’ kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV.
Shabiki mwingine aliuliza: “Pia man water ni mkali au unasemaje master J?”
Na hiki ndicho alichojibu Jay: “mkali lakini hakusahili kushinda mwaka huu”
Swali tofauti na muziki ambalo lilijirudia mara nyingi ni kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake Shaa, shabiki mmoja aliuliza:
“Mnafunga ndoa lini ww na Shaa manake mnapendezana kweli? Au ni mchepuko tu wa lami?
Na jibu la Joachim aka Master J mabibi na mabwana lilikuwa “SOON”.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment