


Taarifa ya kamanda wa Polisi inasema katika ajali hiyo watu 17 wamepoteza maisha kati yao wanaume ni 12 na wanawake ni 5,Pia watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali za wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari jingine na kwenda kuligonga basi hilo
0 MAONI YAKO:
Post a Comment