July 31, 2014

maporomoko India
Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia katika kijiji cha kijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Vikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya kuwanusuru waliofukiwa na maporomoko ya udogo huo, japo kuwa mazingira magumu na hali mbaya ya hewa vinakwamisha shughuli hiyo.Maporomoko hayo yaliyokikumba kijiji cha Malin India karibu na jimbo la Maharashtra yamesababisha nyumba nyingi kusombwa huku watu wakihofiwa kunaswa pia katika eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Devidas Desh pande aliyepo katika eneo la tukio anasema jingo pekee linaloonekana kunusurika na janga hilo ni ya shule pekee, huku maeneo mengine yakiwa tambarale kabisa.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.

Maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea nchini India hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo hunyesha kuanzia mwezi june hadi septemba kila mwaka.

Related Posts:

  • UN yailaumu Tanzania kwa hali ilivyo DRC   Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu Tanzania kwa kuwaruhu… Read More
  • Mbasha asita kuzungumzia mtoto wa mkewe    Mwimbaji wa miondoko ya injili nchini, Emmanuel Mbasha hatimaye amefunguka juu ya mtoto ambaye mkewe Flora Mbasha amejifungua na kuweka wazi kuwa, kwa sasa asingependa kusema chochote juu yake mpaka pale wa… Read More
  • Cindy Sanyu amponda Miss Uganda live   Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Cindy Sanyu ameibua mjadala mzito mtandaoni baada ya kufunguka wazi kuwa mrembo anayeshikilia taji la miss Uganda kwa sasa, Leah Kalanguka ana muonekano mbaya, na kukazia … Read More
  • Ngassa ajutia nafasi, ailalamikia Yanga   Na Richard Bakana, Dar es salaam MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mrisho Ngassa, amejutia uamuzi wake wa kukataa kujiunga na El Merreikh ya Sudan akisema kuwa yalikuwa ni… Read More
  • Picha za Wema Sepetu na Ommy Dimpoz, zilipigwa usiku wa manane    Zile picha za mahaba zilizosambaa kwenye mitandao zikimuonyesha Staa wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz na Wema Sepetu wakiwa kitandani zimezidi kuzua utata baada ya Ommy kusema hakujua alipigwa saa ngapi kwani hak… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE