Staa
katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
Chanzo makini
kilichopo ndani ya kamati ya wasanii hao wa Bongo Movies, kitendo cha
Taasisi ya Twaweza kutangaza kuwa Lowassa anaongoza na kuwagaragaza
makada wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwao ni ishara tosha
ya ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao.
SIKU chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangazwa
kuwa anaongoza katika kinyang’anyiro cha urais 2015, mastaa mbalimbali
wanaomuunga mkono wameandaa mkakati wa kumfanyia sherehe ya kumpongeza.
“Mastaa wa Bongo Movies wanaomuunga mkono Lowassa wameandaa bonge la
pati la kumpongeza Lowassa na siku hiyo watakula, watakunywa maana
mipango yao tayari wanaona inakwenda vizuri na hakuna mtu ambaye anaweza
kumuangusha katika chama hicho,” kilisema chanzo bila kutaja lini na
wapi watakapofanyia sherehe hiyo.

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Esha Buheti.
Mbali na sherehe hiyo kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, chanzo hicho
kimeeleza kuwa wanatarajiwa pia kualikwa wananchi mbalimbali wanaomuunga
mkono Lowassa.
“Safari ya kuelekea uchaguzi mkuu ndiyo imeanza rasmi, Twaweza
wametafiti na kubaini kile ambacho sisi tulikuwa tunakiamini, Lowassa
hana mpinzani CCM, ushindi ni lazima,” kilisema chanzo hicho.

Staa
katika tasnia ya filamu Bongo, Mahsein Awadhi.
Wasanii ambao wanatajwa
kuwa upande wa Lowassa ni Jacqueline Wolper, Esha Buheti, Mahsein Awadhi
‘Dk. Cheni’, Wema Sepetu ‘Madam’ na wengine kibao. Taasisi ya Twaweza
iliyofanya utafiti kwa mwezi Septemba, ilitangaza matokeo hayo Jumatano
iliyopita na mtafiti wake, Elvis Mushi ambapo alisema wananchi 1,445
walihojiwa kwa njia ya simu ambapo Lowassa alipata asilimia 13 huku
waziri mkuu wa sasa, Mizengo Pinda akimfuatia kwa kupata asilimia 12.

Wema
Sepetu ‘Madam.
Wengine waliopigiwa kura katika utafiti huo ni Katibu
Mkuu wa Chadema, Wilbrod Slaa aliyepata asilimia 11, Mwenyekiti wa CUF,
Profesa Ibrahim Lipumba akipata asilimia 6 huku Waziri wa Mambo ya Nje,
Bernard Membe akiondoka na asilimia 5.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment