Diamond na Davido wana beef? Hili ni swali
ambalo watu wengi bado hawajapata jibu lake hasa baada ya wiki hii
Davido kutweet maneno yaliyohisiwa kuwa yanamlenga Diamond.
Akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds
FM Ijumaa hii, meneja wa Diamond, Babu Tale amesema Diamond na Davido
sio washkaji ila wana mahusiano ya kibiashara tu.
“Hakuna vita mimi na menejimenti ya Davido, Tunaongea,” amesema Tale.
“Hapa ninaweza nikakuonesha meseji za mimi na
Kamala ambaye ni meneja wa Davido. Nikinukuu maneno ya Kamala kwangu
ile meseji ambayo Davido aliposti ya kwanza hakuwa anamface Diamond
according to Kamala. Akaniambia mbona ‘watanzania wameelewa vibaya’
nikamwambia ‘tuliache hili limepita na limeshatokea hatuwezi kuwaambia
bana Davido hajaongea hivi kwa maana hii, tutafute njia nyingine ambayo
Davido anaweza akasehewa na Watanzania,” ameongeza Tale.
“Lakini sitaki kuamini kama Davido na Diamond
wana vita. Juzi Davido alikuwa anaposti vitu vyake sio kwa sababu ya
Diamond. Watanzania wote washaanza kusema ‘oooh Davido ashaanza
kumtukana Diamond’. Nikwambie kitu kimoja Diamond hata baada ya kufanya
ile video huwaga hawachati, Diamond akimtaka Davido ataniambia mimi au
atamwambia Salam au Kamala.”
0 MAONI YAKO:
Post a Comment