January 10, 2015


aff6SAM_3898 kovaaaaaaaaaaaaa
Moja ya story ambazo zimechukua headlines siku ya jana  ni ishu ya watu kadhaa kulalamikia kwamba picha zao zimeonekana kwamba wao ni watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa kujihusisha na kundi la Panya Road.
 Katika kipindi cha XXL ya Clouds FM, Kamanda wa Polisi Suleiman  Kova ameongelea story hiyo; Kuna mtu aliniuliza swali siku ya leo, mimi mwenyewe nilitoa picha tatu kwamba hao ndio realy leaders ile ya Press Conference tuliyofanya, baada ya hapo sijatoa tena picha nyingine, isipokuwa ninachofahamu mimi ni kwamba badae nikaona kwenye gazeti hilo kuna picha yangu mimi ambayo sikupigwa siku hiyo au jana yake nikaona kuna picha nyingine, zote ni za zamani hizo.
Sasa inawezekana mle ndani huyo kijana yumo lakini jibu ni kwamba hiyo ni kazi ya waandishi wa habari… yani ninyi huwa mna taratibu zenu kwamba likitokea tukio fulani labda liwe la michezo au la vita mnachukua background picha ambazo zipo unaona sasa mimi tena siwezi kulaumiwa kwamba eti hizo picha zinanihusu mimi, mbona hata mimi ya kwangu ilitoka nikiwa na cheo cha Senior Assistant Commissioner… lakini nimekubali tu kwa sababu najua cha muhimu pale ni message kwa wananchi kwamba kuna suala la panya road na hata kuna wengine walishakamatwa siku za nyuma.
Kwa hiyo sisi Polisi hatuwezi kuendelea kulaumiwa kwamba kwa nini hizo picha zimeonekana… sie hatujazipeleka, tulizozipeleka ni tatu tu ambazo hao watu hawajalalamika, kwa hiyo kama wakitaka huyo bwana aulizwe kwanini wamemchapisha kwanza nyinyi sasa ndio mnatakiwa muwaeleweshe hawa raia kwamba hizo picha ni kawaida yetu sisi huwa tunazitoa hivyo ilimradi ni ishu ambazo zina mahusiano, unakuta mmetoa picha za Rais za miaka mitatu iliyopita au Waziri… au mtu yoyote yule unatoa kwani ukitoa zile atasema mbona sijapigwa picha?“– Suleiman Kova.


Related Posts:

  • Brand New Video: Muda wetu - Nay True Boy   Nay True Boy ametuletea Video ya wimbo wake mpya kabisa inaitwa Muda wetu. Audio ya wimbo huu imefanywa katika studio za free nation chini ya producer Awsome huku Video ikifanywa na Director Abel Dedo.   … Read More
  • Tuhuma za madawa ya kulevya, Yusuph Manji afikishwa Mahakamani   Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji, akiingia Mahakama ya Kisutu leo mchana baada ya kuwasili mahakamani hapo kwa ajili ya kupandishwa Kizimbani kujibu mashitaka.Manji baada ya kupanda mahakamni alisomewa shitaka l… Read More
  • Kajumulo kufungua maduka ya vifaa vya michezo nchini   Mwanamichezo aliyewahi kutamba kipindi cha nyuma nchini Tanzania Alex Kajumulo, yupo katika hatua za mwisho za kufungua maduka yake ya vifaa vya michezo nchini Tanzania. Alex Kajumulo anayemiliki kampuni ya Kajumo… Read More
  • Waliokamatwa kwa Dawa za Kulevya Wafikia 349 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya kukamatwa kwa jumla watuhumiwa 349 akiwemo 'video queen' Agnes Gerald maarufu kwa jina la 'Masogange', katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaohusika na d… Read More
  • Diamond ajisalimisha polisi   Mfalme wa nyimbo za Bongo fleva Diamond Platnum, leo hii ameitwa kituo cha polisi. Kupitia katika ukurasa wake wa Instagram Diamond ameeleza kile kilichomfanya akaitwa polisi. Leo nilireport kituo kikuu cha pol… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE