Salman bin Abdulaziz al-Saud, ndugu wa
Abdullah na mtoto wa mwanzilishi wa ufalme, hatimaye ni mfalme wa Saudi
Arabia na mlinzi wa maeneo mawili takatifu ya Uislamu.
Ijumaa, Januari 23, baada ya kutangazwa kifo cha Abdullah,
mfalme Salman aliitisha mara moja kikao cha Baraza la utawala wa kifalme
na kuteuliwa ndugu yake mwingine, Moqren, kama mrithi wake.
Wakati huo huo mfalme Salman ameongea kwenye televisheni ya taifa
akihakikishia ulimwengu na raia wa Saudia mwendelezo wa utawala wa
kifalme na sera zake.
Katika hotuba yake ya kwanza ya mfalme, Salman wa Saudi Arabia,
mwenye umri wa miaka 79, amethibitisha kwamba hakutakuwa na mabadiliko
katika siasa za nchi.
" Sisi tutakaa na nguvu ya Mungu, kwenye njia ya haki ambayo
taifa hili lilifuata tangu kuanzishwa kwake na mfalme Abdul Aziz bin
Saud na wanawe baada yake", amesema mfalme Salman.
" Mungu alitaka mimi nipewe majukumu haya makubwa, naomba kwa Mungu anipe msaada huo", ameongeza mfalme Salman.
Saudi Arabia ni nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa mafuta. Uzalishaji
wake wa dhahabu nyeusi unalinda ushawishi wa shirikisho la la nchi
zinazouza mafuta (Opep). Saudi Arabia pia ni mchangiaji muhimu katika
mahusiano na Mashariki ya Kati, hasa katika miaka ya hivi karibuni.
Riyadh ni mshirika muhimu wa Marekani na nchi za Magharibi katika sekta
ya kidiplomasia.
Serikali ya Saudi Arabia ina mwelekeo wa Kiislamu. Mfalme mpya ametoa
wito kwa umoja miongoni mwa Waislamu ambao wamegawanyika kutokana na
vita vinavuendelea duniani.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment