
Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill
Gates amekunywa maji yaliotengezwa kutokana na kinyesi cha binaadamu
kama maonyesho ya teknologia mpya itakayoweza kutoa maji safi katika
mataifa yanayoendelea.
Mwanzilishi huyo wa Microsoft amesema kuwa
ataisambaza mitambo ya teknologia hiyo mpya kote duniani baada ya
kuifanyia majaribio mwishoni mwa mwaka huu.Teknologia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji.
Kulingana na shirika hilo la hisani takriban watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.
katika kanda ya video iliowekwa katika blogi yake,Bwana Bill Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe.
''Maji hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote yale niliokunywa,na baada ya kusomea teknologia hii nitayanya kila siku.
Maji haya ni salama kabisa'',aliandika katika blogi yake.Kulingana na mtengenezaji wa mtambo huo Peter Janicki,maji taka hayo huchemshwa kabla ya mvuke wa maji hayo kutengwa na taka ngumu.
Taka hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke unaoendesha mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakaazi wa eneo hilo.
Maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji ili kutoa maji safi ya kunywa.
''lakini kwa nini mtu awe na wazo la kubadilisha uchafu kuwa maji ya kunywa na umeme'',aliuliza Gates.
Jibu aliloandika ni kwamba kwa sababu magonjwa yanayosababishwa na mazingira machafu huwaua watoto 700,000 kila mwaka na huwakinga wengine wengi dhidi ya kuathirika kiakili na kimwili.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment